fbpx

Kampuni iliyosajiliwa nchini Estonia, FiFi Finance, imeanzisha tovuti ya kifedha ya Kiswahili ili kusaidia wazungumzaji wa Kiswahili kupata habari, elimu na maarifa kuhusu masuala mbalimbali ya fedha ili kuboresha maisha yao.

Kiswahili kinazungumzwa zaidi na watu milioni 150. Kati ya nchi ambazo Kiswahili kinazungumzwa ni pamoja na Tanzania, Kenya, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Somalia, Zambia, Malawi na Visiwa vya Komoro.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, elimu ya kifedha ni moja ya nguzo muhimu za ustawi wa kijamii na kiuchumi barani Afrika na duniani kote.

Kampuni ya FiFi Finance ilianzishwa Machi 2019 na wavuti ya FiFi ya Kiswahili ilianzishwa rasmi Julai 2019.

Habari Bora Za Kifedha

Habari zinazochapishwa kwenye wavuti hii zinalenga watu binafsi, walaji na biashara ndogo na za wastani katika nchi husika. Makala zake zinajibu maswali mbalimbali ya masuala ya kifedha kama vile: Je ni vipi ninaweza kuwekeza na kupata mapato kila mwezi? Ni jinsi gani ninaweza kuwekeza kwenye Soko la Hisa la Dar Es Salaam?

Habari nyingine muafaka katika tovuti hii ni pamoja na: Nitawezaje kuanzisha biashara mtandaoni? Wapi ninaweza kupata wawekezaji kwenye nyanja ya ujasiriamali? Au habari za mikopo kama vile: Ni wapi ninaweza kupata mikopo nafuu au isiyo na riba? uduma zipi zinatoa mikopo kwa njia ya simu au mtandaoni?.

Tovuti hii pia inatilia mkazo habari za ushauri kuhusu njia nafuu na za haraka za kutuma fedha nchini Tanzania toka nje ya nchi na pia habari kuhusu Bitcoin kama moja ya njia ya uwekezaji fedha binafsi. 

Lengo la muda mrefu la FiFi Finance kwa lugha ya Kiswahili ni kuifanya tovuti hii kuwa wavuti bora na ya kuaminika katika masuala ya kifedha.

READ MORE:  Jinsi ya Kutumia WhatsApp Business Kukuza na Kutangaza Biashara Yako

Kukuza Lugha na Habari za Kiswahili

Zaidi na tovuti hii ya Kiswahili, kampuni hii chipukizi ina nia ya kukuza maarifa na zana za lugha ya Kiswahili mtandaoni. Katika kutekeleza lengo hili, FiFi Finance imegharamia utafsiri wa zana huria ya kublogu ya WordPress. Hivi sasa wanablogu wa Kiswahili wanaweza kujenga blogu kamili ya Kiswahili kwa kutumia toleo la WordPress la Kiswahili, jambo ambalo halikuwezekana hapo awali.

Kusaidia Kutafsiri Habari za Kitabibu

Pamoja na habari za kifedha, FiFi Finance inaamini kuwa ni muhimu kwa habari za kitabibu kupatikana mtandaoni kwa lugha za kienyeji kama vile Kiswahili. Kwahiyo, FiFi Finance imetoa tangazo la kuwataka watafsiri wa Kiswahili kushiriki katika mradi wake wa kutafsiri makala za matibabu zilizoko kwenye Wikipedia ya Kiingereza kwenye Wikipedia ya Kiswahili. Watafsiri hawa watalipwa kwa kazi hiyo.

Nia ya mpango huu ni kuunda hifadhidata ya matibabu kwa ajili ya kusaidia wanafunzi, wakunga, waganga wa asili, na umma kwa ujumla. Mpango huu utasaidia pia kupambana na habari bandia mtandaoni kuhusu matibabu. 

Ujumuishaji wa Shughuli za Kifedha Duniani

Ukiachilia wavuti ya Kiswahili, FiFi Finance ina wavuti katika lugha za Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kireno, Kihispania na Kiholanzi. 

FiFi Finance ilianzishwa na mradi wa SEO Crew OÜ. Hivi sasa ina waandishi zaidi ya kumi, pamoja na wahariri na watafsiri.

FiFi Finance inatarajia kujenga tovuti za lugha nyingi zaidi ikiwa ni pamoja na lugha za Kiafrika. Kwa kufanya hivyo, kampuni hii ina lengo la kulipa kipaumbele suala la ujumuishaji wa shughuli za kifedha barani Afrika. 

.