Jinsi ya kukuza biashara yako kupitia mtandao (Digital Marketing)

components of doigital marketing

Written by Shukuru Amos

I am the founder of Tanzlite Digital, Creator, Author of Mbele Ya Muda, and the most followed Tanzanian marketer on LinkedIn.

Posted August 31, 2019

Biashara na matangazo ya karne ya 21 yanategemea sana teknolojia. Tunaishi ulimwengu wa dijitiali hivyo kila kitu hakina budi kufanywa kidijitali.

Unaweza kuwa na biashara yako au kampuni yako inayotoa huduma ama bidhaa imara na uhakika kabisa lakini usipotumia bidii kujitangaza ama kujiweka online, unaweza kuzidiwa na watu ambao huduma zao hazina ubora zaidi yako.

Kujitangaza (au kutafuta masoko) kimtandao ni njia rahisi na isiyo gharama kuwafikia watu wengi zaidi. Ukweli ni kwamba usipofanya matangazo ya biashara yako, yote uyafanyao yataishia kwa watu wachache tu wanaokuzunguka.

Nenda na wakati

Siku hizi mtu akitaka msaada wa jambo fulani wazo la kwanza kumjia ni kushika simu yake na kuperuzi kuhusu akitakacho. Hapo ndipo huweza kukutana na majibu ya swala alitakalo mtandaoni.

Fikiria wewe ndiyo hauko mtandaoni, mtumiaji huyu wa internet atakufahamu vipi? Atafahamu vipi una duka la nguo Kariakoo? Badilika. Nenda na wakati, hamia ulimwengu wa digitali. Wazungu wanaita ‘Digital Marketing’ mbinu ya kutafuta masoko na kujitangaza kupitia majukwaa ya kimtandao kama vile tovuti, mitandao ya kijamii, email, whatsapp na kadhalika.

Unaanzia wapi?

Ni rahisi. Ingawa  waweza kutumia pesa panapohitajika, kujitangaza mitandaoni ni bure kabisa. Ni kama vile ulivyo na akaunti facebook bila malipo yoyote. Cha msingi ni wewe kujifunza mbinu za uendeshaji na kuchagua njia ipi inakufaa zaidi

Miliki tovuti/website yako

Tovuti hasa kwa mashirika, makampuni na biashara kubwa ni kitu cha lazima. Hii huongeza hadhi ya kampuni kwa ujumla. Tofauti kubwa kati ya tovuti ama website na mitandao mingine ya kijamii ni namna ya kuweka maudhui.

Kupitia tovuti, mtu anaweza kupata taarifa kwa kina kuhusu kampuni au bidhaa. Pia kwenye tovuti kunaweza kufanyika shughuli kama manunuzi ya mtandaoni, kuandikisha watu kwa ajili ya program, newsletter na kadhalika.

Unatengenezaje tovuti? Ni rahisi. Kuna watu na makampuni mengi yapo kukusaidia kufungua tovuti yako. Sisi Kampuni ya Tanzlite Digital tunatengeneza website za kisasa kwa bei nafuu ili kukusaidie wewe na biashara yako katika ulimwengu wa digitali.

ALSO READ:  Mambo Matano Mwanachuo Anaweza Kufanya ili Kukwepa Unemployed Baadae

Mitandao ya kijamii

Karibia kila mtu yuko Facebook au Instagram. Maana yake ni kwamba soko liko huko kwa sababu ndiko watu waliko. Cha kufanya ni kupeleka biashara yako huko. Fungua akaunti kwa jina la biashara au kampuni yako na uanze kujitangaza.

Nini cha kupost ukiwa huko? Hapa ndipo wengi hukosea. Makampuni mengi hapa nchini hayafahamu namna ya kutumia mitandao ya kijamii.

Mitandao ya kijamii ni watu, hivyo wewe kama kampuni unatakiwa ufahamu namna ya kuishi na watu. Fahamu namna ya kushirikiana na watu. Isiwe kila siku unapost kuhusu wewe na bidhaa zako tu. Utawachosha watu. Kuwa mbunifu.

Unaweza ukawa unapost picha za bidhaa zako, picha za wateja wenye nyuso za kuridhika na huduma yako. Kama utakuwa mtundu zaidi waweza tengeneza vipande vifupi vya video. Kumbuka pia hautakiwi kupost mara kwa mara ikawa too much.

Jambo la msingi kuzingatia ni kwamba mitandao ya kijamii ni majukwaa tofauti tofauti yenye maudhui na makundi ya watu tofauti. Ni muhimu kulifahamu hili ili aweze kutambua kipi cha kufanya ukiwa kwenye haya majukwaa.

Boosti tangazo lako kupitia Sponsored Ads

Kama ndiyo kwanza unaanza na wateja hawakuji na huna followers wengi, njia rahisi ya kufikia watu ili waone unachouza ni kulipia tangazo. Kama huwa unaona post ya page ambayo huja-follow imeandikwa “Sponsored”, basi hayo ndiyo matangazo ya kulipia. Bei ya kutangaza ni rahisi tu; kwa upande wa Facebook na Instagram kiwango cha chini ni dola moja tu (Tsh 2400*)

WhatsApp pia ni fursa kubwa

Kwa kaiwaida WhatsApp hujumuishwa kwenye kundi la mitandao ya kijamii. Lakini kiuchambuzi zaidi, WhatsApp pamoja na majukwaa mengine kama Telegram na Messenger yanaitwa private messaging platforms. WhatsApp imekuwa kimbilio la wajasiriamali wengi wa kitanzania. Kupitia magrupu na status whatsapp, watu wanatangaza bidhaa zao na kupata wanunuzi. Soma zaidi jinsi ya kutumia WhatsApp Business hapa

ALSO READ:  Je mtandao wa kijamii wa TikTok waweza kuwa fursa kwa biashara?

Weka biashara yako kwenye Google My Business

Kampuni ya Google wana mfumo wa kukuwezesha kuweka biashara yako kwenye ramani ya Google ili watu wa karibu na eneo lako waweze kukuona wakitafuta huduma au bidhaa inayoendana na yako. Pia wanaweza kuacha maoni kama vile kukupa five star rate ili kuongeza visibility yako mtandaoni.

Pia zipo tovuti zingine zinazokuwezesha kuorodhozesha biashara au bidhaa yako kama vile Kupatana, na Zoom Tanzania.

Kuwa mbunifu katika maudhui (Content Marketing)

Karibia kila mtu anaandika maudhui mtandaoni. Iwe ni mstari mmoja kama status za facebook na whatsapp laikini yote ni maudhui. Kinachokuja kutofautisha kati ya maudhui mengi yanayoandikwa kila siku mtandaoni ni aina na stadi za uandaaji maudhui hayo.

Nichukulie mfano wa mchekeshaji maarufu nchini, Idris Sultani, kuna wakati huandika posts kwenye ukurasa wake wa instagram akitangaza makampuni kama Uber. Uandishi wake ni mwepesi na wenye ucheshi, lakini hapo ameweza kutangaza biashara.

Kwa makampuni na taasisi mbalimbali unaweza kuajiri muandaa maudhui na mwongozaji wa akaunti za kijamii za kampuni. Hili ni jambo muhimu sana katika ulimwengu wa mawasiliano ya kidigitali.

Kampuni yetu ina wataalamu wa masuala ya Digital Marketing ambao wanaweza kukurahishia kazi kuandaa yote haya. Kazi yako ni kufanya biashara, sisi tunaimarisha uwepo wako mtandaoni (online visibility)

Amua sasa!

Siku hizi mambo yanaenda kidigitali, hivyo hata biashara yako haina budi kuenda na wakati.

Kama uliwahi kujaribu tovuti au mitandao ya kijamii na haukupata matokeo mazuri basi kuna mahali haukufanya kwa usahihi. Tafuta wataalamu wakusaidie. Unapitwa wateja kwa kushindwa kuwa online. Amua sasa!

TANGAZO: Tumeanzisha group la WhatsApp kuwapa USHAURI Wajasiariamali wanaouza bidhaa mtandaoni kama vile Instagram, Facebook na WhatsApp. Bofya picha hapo chini.

12 Comments

  1. emmanuel tang'ale

    I like it

    Reply
  2. emmanuel tang'ale

    To improve my business on Milk production

    Reply
    • Shukuru Amos

      Hello Emmanuel, could you please tell us more about your business? We would love to help you take it to the next level by growing exposure and acquiring new customers.

      Reply
      • Medrick buttama

        I have a business concerns medical drugs xo hw can I promot through online market?

        Reply
      • Nyakisasa Empire

        We are doing brokerage services in Arusha. Inc. Real estate, car selling, debt collection, car hiring and others alike. Would you mind on how you can help my businesses?

        Reply
      • Aslatu

        This lesson is productive, thank you.

        Reply
    • Abdallah Mtalika

      Nimeaza kufanya matangazo ya bidhaa yangu ya mdawa kupitia mitandao ya kijamii hususan WhatsApp na Facebook lakini naona mwanzo wangu haujapenda vizuri, ni nini natakiwa kufanya ili kuakikisha inaenda vizuri

      Reply
  3. Makongo marketing

    Thank for opening me..

    Reply
    • Dismas Chacha

      Thanks for open,support and improve my brain capacity

      Reply
  4. Amos malale

    You add something great in my mind.
    in like it

    Reply
  5. Grida msukwa

    Well noted. Thanks for great lesson hope if I try I get great results as described

    Reply

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

You May Also Like

Products From Tanzlite