Idadi ya Watanzania wanaotumia internet imefikia milioni 27. Katika mamilioni haya ya watu, kuna wateja wengi sana kwa ajili ya biashara yako. Lakini UNAWAPATAJE? Au wanakupataje? 🤔
Kabla hujaanza kutumia njia yoyote ya kidigitali kupata wateja mtandaoni, ni vyema ukafahamu makundi matatu ya wateja wanaopatikana mtandaoni. Itakusaidia kuandaa mpango (digital strategy) utakaoleta matokeo mazuri.
Makundi Matatu ya Wateja Mtandaoni
1.Wateja wanao kufahamu: hawa ni wale ambao tayari wanajua biashara yako. Wanaweza kuwa ni followers kwenye account zako za mitandao ya kijamii, au una email list yao au wame-subacribe kupata huduma yako.
Hawa ni rahisi kuwauzia bidhaa yako. Watu wakikufollow ujue tayari wamevutiwa na unachokifanya.
Kazi yako ni kuwapa huduma bora ili wakakutangaze kwa wenzao. Fanya kila uwezalo kuhakikisha hili kundi haliondoki (Customer Retention)
2. Kundi la pili ni wateja wanaohitaji bidhaa yako lakini hawakujui. Hawa wanaweza kuwa wanapata bidhaa hiyo kutoka kwa mtu mwingine au hawajui wapi pa kuipata.
Kama wanaipata bidhaa hiyo kutoka kwa mtu mwingine maana yake tayari una mshindani. Hapa unakuwa na kazi ya ziada ya kumchunguza mshindani wako. Anatumia mbinu gani kupata wateja na bidhaa yake ni bora kiasi gani kulinganisha na yakwako.
Je anatumia influencers? Maudhui yake ni bora kiasi gani? Ni mtandao gani wa kijamii amejikita zaidi? Ukifahamu haya na mengine utaweza kuja na mkakati (digital strategy) imara wa kukuza biashara yako.
Kwa kuwa kundi hili ni la watu wenye UELEWA juu ya wanachohitaji, wengi hutumia search engines kutafuta bidhaa hiyo (they are actively searching online). Hivyo njia nyingine ya kuwapata ni kuwa na mpango imara wa SEO (Search Engine Optimization) au kutumia matangazo ya Google Ads.
3.Kundi la tatu ni la wale ambao wangependa kutumia bidhaa yako lakini hawajui kama wanahitaji (they don’t know if they need it). Hapa sasa inabidi uwe vizuri kwenye kitu tunaita Content Marketing. Kundi hili la wateja wanahitaji kuelimishwa sana kabla hawajafanya maamuzi ya kutoa hela yao kununua huduma yako. Wanahitaji elimu juu ya tatizo walilo nalo na kwamba kuna suluhu ya tatizo hilo ambayo ni hiyo bidhaa yako.
Mara nyingi ukiwa umegundua solution mpya juu ya tatizo fulani, tuseme ni software, tiba lishe au kitu chochote —watumiaji wa solution yako mara nyingi wanakuwa kwenye hili kundi la tatu. Wanahitaji maudhui ya kutosha kuwafundisha tatizo lililopo, madhara ya tatizo hilo na faida za kutumia bidhaa yako.
Hitimisho
Kumbuka biashara ni watu. Kufahamu makundi ya wateja na tabia zao mtandaoni itakusaidia kuandaa mpango wa digitali wenye kuleta mafanikio katika biashara yako. Hasa upande wa maudhui kwani makundi haya matatu yanahitaji aina tofauti ya maudhui.
Ukiwapa huduma bora wateja waliopo kwenye kundi la kwanza hapo juu, wanaweza kuwa mabalozi wazuri kwa wateja wa kundi la pili na la tatu.
Natumaini makala hii imekusaidia. Naitwa Shukuru, ni mwandishi na mtaalamu wa Digital Marketing. Nipate kupitia mtandao wa WhatsApp hapa. Au jiunge na group letu la Wafanyabiashara wadogo mtandaoni kwa Tsh 7500.
Maisha yanakimbia kwa kasi sana. Miji inazidi kuwa ya kisasa na yenye kupendeza. Umri nao unatutupa mkono vilevile.
Siku hizi ukilala, ukiamka kuna jambo jipya limeibuka. Mitindo tofauti tofauti ya mavazi, muziki na mengine inakuja na kuondoka kama maji yatiririkayo chini ya daraja la mto uendao kasi.
Ukija upande wa teknolojia ndio usiseme kabisa. Leo iPhone imetoka mpya kesho Samsung katoa kitu kikali zaidi. Hujakaa sawa Huawei anamtikisa Mmarekani kwa teknolojia ya 5G. Hapa tunaoteseka ni sisi. Hela zenyewe ziko wapi za kuweza kuwa na kila toleo jipya? Wacha tubaki na tecno zetu bwana!
Ninafahamu unatumia mitandao ya kijamii hasa ile maarufu kama Instagram, Facebook na Twitter. Huenda ukawa umekutana na makala hii kwenye moja ya mitandao hiyo.
Lakini kuna mtandao mmoja unakuja kwa kasi sana kwa sasa. Unaitwa TikTok. Endelea kusoma kuona ni nini kipya juu ya mtandao huu.
Takwimu zinasemaje kuhusu mtandao wa TikTok?
Kwa kipindi cha miaka minne tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016, TikTok imeweza kuwa na watumiaji zaidi ya milioni 500 duniani kote. Wengi wa watumiaji hawa wakiwa ni vijana.
Ripoti ya Globalwebindex ya mwaka 2019, inaonyesha asilimia 41 ya watumiaji wa TikTok wana umri kati ya miaka 16 na 24 (Globalwebindex, 2019). Kati ya watumiaji hao, watu zaidi ya milioni 150 hutumia application hiyo kwa siku.
TikTok inawapa watumiaji uhuru wa kutengeneza vipande vifupi vya video (visivyozidi sekunde 15) vikinakshiwa na nyimbo na urembo mwingine (filters) wa kuvutia kwa kutumia simu zao za mkononi. Video hizi zimejaa furaha na ucheshi (funny).
Ukitofautisha na mitandao mingine kama Twitter na Instagram, mitambo (algorithm) ya TikTok inakuonesha vitu unavyovitaka tu. Sio mara unakutana na post ambayo hata hujui imetoka wapi kama inavyotokea huko Twitter na Insta. Pia matumizi ya hashtag yanatamba sana kwenye mitandao huu.
Ukiitizama vizuri application ya TikTok utaona ina muonekano sawasawa na application inayoitwa Musical.ly. Hii ni kwa sababu TikTok ambayo ni kampuni ya Kichina, iliinunua application ya Musical.ly ili kuweza kuwafikia watu wengi hasa vijana wa kimarekani.
Swali; Je TikTok inaweza kuwa fursa mpya kwa wafanyabiashara?
Kwasasa TikTok haina mfumo wowote unaowezesha kuweka matangazo ya kulipia (sponsored ads) kama tunayoyaona huko kwenye mitandao mingine.
Lakini kama tunavyofahamu, hakuna kitu cha bure. Nionavyo mimi, jukwaa hili halitakuwa la bure kwa mda mrefu.
Kwa kuwa mtandao huu unapendwa na vijana wengi ambao ndio wenye nguvu ya ushawishi katika masoko, ninaona kuna kila dalili ya makampuni makubwa (brands) kuishawishi ikubali TikTok ikubali matangazo.
Baadhi ya takwimu zinatabiri mtandao wa TikTok utakuja kuteka na kuizidi mitandao kama vile Instagram na Snapchat.
Changamoto kubwa ya mitandao ya kijamii ni tabia yake ya kubadilika kila mara, kwa kuja na mifumo mipya au kupotea kabisa kama mtandao uliokuwa ukimilikiwa na kampuni ya Google, uliofahamika kwa jina la Google+.
Lakini pia ni lazima tukubaliane na ukweli kwamba hatuwezi kukwepa social media. Mitandao hii imewapa nguvu watumiaji kuwa na uhuru wa kuchagua ni namna gani wanataka kupokea taarifa. Hivyo kama mfanyabiashara unaetafuta kukuza jina la biashara yako na kufikia wateja wengi zaidi, huna budi kuwekeza kwenye moja ya mitandao hii.
Palipo na wengi pana fursa nyingi. Wewe kama mfanyabiashara, unajiona uko tayari kuwafata wateja wako walioko TikTok? Au utawasubiri wakirudi Insta na Fb?
Mwanafalsafa maarufu wa Kijerumani, Karl Marx aliwahi kuonya kwamba teknolojia itakuja kuondoa kazi wanazofanya watu. Kwamba watu watakuwa hawana kazi za kufanya.
Hivi karibuni kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, imedhihirika kuwa maono ya msomi huyu hayakuwa sahihi.
Ni kweli kwamba teknolojia imechukua kazi nyingi zilizokuwa zikifanywa na binadamu hasa zile zenye uhitaji mdogo wa kufikiri kama vile kubeba mizigo viwandani. Siku hizi kuna maroboti yanayofanya kazi kwa ufanisi na kwa muda bila kuchoka kuliko binadamu.
Lakini pia kuna ukweli mwingine. Teknolojia imetengeza na kuboresha kazi nyingi zaidi kulinganisha na zile ilizoziondoa. Mojawapo ni hii kazi inaitwa Social Media Marketing. Mtu anayefanya kazi hii anaitwa Social Media Manager, au Social Media Coordinator.
Ulishawahi kujiuliza ni nani huwa anapost kwenye account ya Instagram ya BBC, Millardayo au account za taasisi kama UNICEF? Basi hiyo ndiyo kazi yenyewe tunayoizungumzia hapa.
Social Media ni kipengele mojawapo muhimu katika suala zima la digital marketing.
Kutokana na kukua kwa matumizi ya mitandao ya kijamii miongoni mwa watu, imeweza kushawishi watu na biashara zao kuingia kwenye Social Media kwa lengo la kushirikiana na kukuza uhusiano na wateja wao pamoja na kupata wateja wapya.
Majukumu ya Social Media Manager
Majukumu ya social media manager ni pamoja na kusimamia na kuendesha akaunti za mitandao ya kijamii ya kampuni au watu maarufu celebrities. Haya ni baadhi ya majukumu muhimu;
Kuandaa maudhui (picha, video, maneno) kwa ajili ya kusambaza kwenye mitandao ya kijamii
Kujibu comments na maswali ya followers
Kushiriki (engage) na wafuatiliaji (followers) kwa niaba ya kampuni
Kuandaa promosheni na matangazo ya kulipia (campaigns) ili kufika watu wengi mtandaoni.
Kukuza jina la brand au kampuni
Kujenga na kuimarisha mahusiano mazuri baina ya kampuni na wateja wake
Kuvutia wateja kufuatilia tovuti za kampuni (lead generation)
Ifahamike kwamba kwenye kazi za Social Media, majukumu ya Social Media Manager, Social Media Specialist na Social Media Strategist yanatofautiana. Lakini kwenye makampuni madogo madogo hasa hap Tanzania unaweza ukajikuta unavaa kofia zote hizi peke yako.
Vigezo na mambo muhimu ya kuzingatia ukiwa Social Media Manager
Hauhitaji kuwa na degree kufanya kazi hii, japo baadhi ya waajiri wanaweza kupendelea mtu mwenye elimu ya juu. Jambo zuri ni kwamba unaweza kujifunza mtandaoni kuhusu maarifa haya na kuwa vizuri katika kazi yako.
Lakini mambo muhimu katika kazi hii ni kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu mitandao mbalimbali ya kijamii. Mitandao hii inatofautiana kuanzia aina ya maudhui na watumiaji wake. Kwa Mfano Instagram ni mtandao unaopendwa na vijana, lakini mtandao kama LinkedIn ni jukwaa la wasomi. Kufahamu tofauti hizi kunakuwezesha kujua mbinu za kuwakilisha maudhui kulingana na jukwaa husika.
Mitandao ya kijamii ni watu. Kama unavotakiwa ujifunze kuishinna watu katika maisha halisi basi ndivyo ilivyo pia ukiwa online. Isiwe kila siku unapost biashara yako tu. Watu hawapendi (don’t be too selly). Kuwa mbunifu.
Jifunze kila siku mambo mapya yanayopendwa huko mitandaoni. Usilenge kupata followers tu, bali followers ambao wako interested na unachokifanya. Ukizingatia haya utaleta matokeo yenye kuridhisha kwa mwajiri wako.