Mbinu Mpya Ya Kupata Kazi Ukihitimu Chuo

Mbinu Mpya Ya Kupata Kazi Ukihitimu Chuo

Soko la ajira ni changamoto kubwa inayosumbua vichwa vya wanafunzi wengi hasa wale wanaohitimu vyuo vikuu katika nyakati hizi. Jambo ambalo linafanya vijana wengi wakose imani ya kufanikiwa tena.

Kwanza ijulikane kuwa degree peke yake sio kigezo cha mhitimu kupata kazi kwa sababu wengi huamini akimaliza chuo kazi ni yake japo kwa sasa vijana wameanza kulielewa soko. Kipindi tulichonacho ni kipindi ambacho bila kujiandaa mapema mambo huwa ni magumu sana huko mbeleni, soko la ajira ni gumu.

Mfano TRA walitangaza nafasi za kazi wakitaka watu 1,596 lakini waliojitokeza kuomba nafasi hizo ni 135,027 maana yake watu takribani watu 133,431 walikosa hiyo kazi. Jaribu kufikiria ni kwa jinsi gani wasomi walivyo wengi mtaani na hawa wote wanazisaka hizo kazi.

Ndio maana nasema ni bora kujiandaa mapema wakati bado upo chuo bado huna mambo mengi ya kushughulika nayo.

Hata hivyo, kupenya kwenye soko la ajira ni jambo linalohitaji juhudi, ujuzi na utayari wa mtu mwenyewe. Katika makala hii, tutaangazia jinsi mwanachuo anavyoweza kupenyeza kwenye soko la ajira.

Je, ni nini unachoweza kufanya kama mwanachuo ili kuongeza uwezekano wa kupata kazi?

Mchakato wa kutafuta kazi unapaswa uanze mapema, hata kabla ya kuhitimu. Je wewe ni mwanachuo?

Kama jibu ni Ndiyo, basi unaweza kuanza kutafuta fursa za kazi mapema mtandaoni au kwa kushiriki katika programu, miradi, semina mabli mbali ili upate exposure ya kukutana na watu walioko kwenye field unayoisomea, kuandaa projects ambazo utakuwa unaonyesha watu utakakuwa unakutana nao.

Vile vile angalia na tenga muda vizuri tafuta makampuni yaliyopo karibu uanze kujitolea. Hii itakufanya ukutane na watu ambao yamkini watakuja kuwa daraja zuri kupata kazi pindi tu unapomaliza chuo.

Pia ukianza kujitolea mapema ukiwa chuo utapata uzoefu wa kazi mapema through internship/freelancing ambao utakusaidia kuwa na ujuzi unaohitajika kwenye hili soko letu la ajira.

Ivi ulishawahi kusikia au kuulizwa hili swali, unauzoefu wa miaka mingapi? chukulia ndio tu umemaliza chuo halafu unaingia interview unaulizwa hilo swali, utajibu nini? Hivyo anza mapema kutafuta makampuni ujitolee wakati bado upo chuo atleast utakuwa unauelewa wa hapa na pale.

Soko la ajira linataka nini?

Kwa kuwa dunia inaenda kwa kasi sana kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kitu muhimu kinachohitajika zaidi ni mtu mwenyewe kuwa tayari kuendelea kujifunza kila siku.

Kuwa tayari kuitumia mitandao ya kijamii kujenga uhusiano mzuri na watu lakini pia kutafuta fursa za kazi mbali mbali. Siku hizi hata ukiwa unafahamu mambo kiasi gani kama watu hawakuoni, hawaoni hayo maarifa uliyonayo ni ngumu kupata fursa.

Lazima uonyeshe kile unachokijua ndipo watu watakufuata wakupe kazi.

Muhimu: Kwa dunia tuliyopo, kama mwanachuo ataamua kuitumia vizuri mitandao ya kijamii yaani social media platforms kama Linkedin katika kujiuza (personal branding) basi mtu huyu;

Hatakuwa anatafuta kazi bali kazi zitakuwa zinamtafuta yeye by Shukuru Amos.

Soko linahitaji vijana wenye maarifa ya kufanya kazi fulani, kuna kazi zingine hata hazihitaji cheti kikubwa uwe na uwezo wa kutatua changamoto za kampuni husika au uwezo wa kuisadia kampuni ikaongeza mauzo au kupandisha hadhi yake?

Jinsi gani unaweza kuboresha ujuzi wako, kupata maarifa yanayohitajika katika tasnia uliyopo?

Technolojia inabadilika kwa kasi sana hivyo unaweza kutumia mitandao ya kijamii kufuatilia mabadiliko yanayotokea katika tasnia yako na kujifunza ujuzi mpya kupitia kozi mbalimbali mtandaoni ikiwemo Marketing.

Chuoni utapewa Mwongozo tu hivyo kuna kila sababu za kutafuta maarifa zaidi. “Kama elimu ya chuo itashindwa kukufanya kuwa unachotaka basi Professor Youtube na msaidizi wake Google wanaweza”.

Utajiuliza ni kivipi Youtube au google inaweza kukusaidia kutimiza ndoto zako? Unahitaji tu kujua unataka usome nini then weka bundle YouTube anakufungulia dunia kuwa unachotaka.

Je ni sahihi kuweka wasifu wako mtandaoni?

Kutengeneza wasifu wako mtandaoni kunaweza kukusaidia sana katika harakati za kutafuta kazi. Wasifu huo utakuwa hewani 24/7 unasomwa na watu wa aina tofauti tofauti ikiwemo waajiri wako baadae, wateja wako.

Hivyo ni vyema kuweka mawasiliano yako, barua pepe na nambari ya simu katika kurasa zako ili watu wakikuhitaji iwe rahisi kukupata.

Wasifu wako mtandaoni unaweza kuwa fursa nzuri kwa wateja au waajiri wanaotafuta talents mtandaoni kujua zaidi kuhusu wewe, uwezo wako na kitu unachoweza kuwasaidia.

Iwe ni Twiter, Facebook, au LinkedIn we jiweke as a professional wa kitu fulani huwezi kujua huko mbeleni ni fursa gani unaweza kuipata. Who knows what will happen tomorrow?

Nifanye nini ili nitambulike na niweze kupata kazi?

Kujitangaza ni muhimu sana katika ulimwengu wa kidigitali hasa unapokuwa kwenye harakati za kutafuta kazi.

Wewe Mwanachuo unapaswa kuwa na ujuzi wa kujielezea mwenyewe katika majukwaa ya aina yoyote iwe kwa maandishi au kwa kuongea.

Kujifunza jinsi ya kuwa mbele kiujuzi na kimaarifa kunaweza kukusaidia kuwa na ujasiri, uwezo wa kuwasilisha mawazo, kushawishi waajiri wakupe kazi.

Asilimia 90 ya mazungumzo mtandaoni huwa ni kwenye maandishi hivyo ni bora kuwa vizuri zaidi kwenye uandishi.

Bonus: Mtu awaye yote, mwenye kutafuta afueni ya maisha yake, yambidi afanye bidii na juhudi zote katika kutatua matatizo yanayoisibu tasnia yake.

Nimalizie kwa kusema tatizo la ajira halitakaa liishe bali litaongezeka maradufu.