Soko la ajira limekuwa ni changamoto kubwa kwa wanafunzi wengi wa vyuo vikuu.
Kupata kazi baada ya kuhitimu ndiyo lengo kuu muhimu ambalo wanafunzi karibia wote hujitahidi kulifikia.
Hata hivyo, kupenya kwenye soko la ajira ni jambo linalohitaji juhudi, ujuzi na utayari. Katika makala hii, tutaangazia jinsi mwanachuo anavyoweza kupenyeza kwenye soko la ajira.
Je, ni nini unachoweza kufanya kama mwanachuo ili kuongeza uwezekano wa kupata ajira?
Mchakato wa kutafuta kazi unapaswa uanze mapema, hata kabla ya kuhitimu. Wewe ni mwanachuo?
Ndiyo, basi unaweza kuanza kutafuta fursa za ajira mapema mtandaoni au kwa kushiriki katika programu, kujitolea katika makampuni, miradi, seminar na kujenga uhusiano na wataalamu wa tasnia anayotaka kufanya kazi.
Kupata uzoefu wa kazi mapema itakusaidia kujenga ujuzi na uzoefu unaohitajika kwenye soko la ajira.
Ivi ulishawahi kusikia au kuulizwa hili swali, unauzoefu wa miaka mingapi? na hapo ndio tu umemaliza chuo, Anza mapema ili baadae swali hili lisikusumbue.
Ni nini kinachotarajiwa kutoka kwako katika soko la ajira?
Unaweza kujenga mtandao wako wa kijamii (networking) kwa kuwa na uhusiano mzuri na walimu, wanafunzi wenzako na wataalamu wa tasnia yako. Kupitia mtandao huo, utaweza kupata taarifa za fursa za ajira pale zinapopatikana.
Muhimu: Kwa dunia tuliyopo kama mwanachuo ataamua kuitumia vizuri mitandao ya kijamii yaani social media platforms kama Linkedin katika kujiuza (personal branding) basi mtu huyu hatakuwa anatafuta kazi bali kazi zitakuwa zinamtafuta by Shukuru Amos.
Jinsi gani unaweza kuboresha ujuzi wako na kupata uzoefu unaohitajika katika tasnia uliyopo?
Technolojia inabadilika kwa kasi sana hivyo unaweza kutumia mitandao ya kijamii kufuatilia mabadiliko yanayotokea katika tasnia yako na kujifunza ujuzi mpya kupitia kozi za mtandaoni.
Chuoni utapewa Mwongozo tu hivyo kuna kila sababu za kutafuta maarifa zaidi. “Kama elimu ya chuo itashindwa kukufanya kuwa unachotaka basi Professor Youtube na msaidizi wake Google wanaweza”. Utajiuliza ni kivipi Youtube au google inaweza kukusaidia kutimiza ndoto zako? Fuatilia Makala zetu.
Ni hatua zipi muhimu ambazo unatakiwa kuzingatia wakati wa kuomba kazi na kuandaa wasifu wako?
Kutengeneza wasifu wako mtandaoni kunaweza kusaidia sana katika kupata kazi. Wasifu huo unapaswa kuwa na taarifa zako za kibinafsi, elimu yako, uzoefu wa kazi na ujuzi wako.
Unapaswa pia kuweka taarifa za mawasiliano yako, pamoja na anwani ya barua pepe na nambari ya simu.
Wasifu wako mtandaoni unaweza kuwa fursa nzuri kwa waajiri kujua zaidi kuhusu wewe na uwezo wako. Mtandao unaofanya vizuri kwa sasa ni linkedin.com
Jinsi gani unaweza kujifunza namna ya kuandaa wasifu wa kuvutia na kufanya mahojiano ya kazi kwa ufanisi?
Kujitangaza ni muhimu katika kutafuta kazi. Kama Mwanachuo unapaswa kuwa na ujuzi wa kujielezea mwenyewe katika majukwaa ya aina yote.
Uwe na uweza kutumia mitandao ya kijamii kuwasiliana na wataalamu wa tasnia yake na kuuliza maswali kuhusu jinsi ya kujitangaza vizuri kwenye soko la ajira.
Kujifunza jinsi ya kuwa mbele kiujuzi na kimaarifa kunaweza kumsaidia mwanachuo kuwa na ujasiri na kuweza kushawishi waajiri kumpa fursa ya ajira.
Asilimia 90 ya mazungumzo ya mtandaoni huwa ni kwenye maandishi hivyo ni bora kuwa vizuri zaidi kwenye uandishi.
Bonus: Mtu awaye yote, mwenye kutafuta afueni ya maisha yake, yambidi afanye bidii na juhudi zote katika kutatua matatizo yanayoisibu tasnia yake.