Hauhitaji tena Kwenda Bank kufungua akaunti ili upate Master card itakayokuwezesha kufanya malipo mtandaoni, hapa kikubwa una akaunti ya M-Pesa.
Au kama unataka usitumie kadi yako unayoitumia kila siku pengine ndiyo hiyo unayotumia kupokea mshahara basi chukua simu yako, fuatana nami katika makala hii itakayokusadia kufahamu jinsi ya kutengeneza Mpesa VISA card hatua kwa hatua.
Uzuri wake ni kuwa hakuna gharama yoyote utakayotozwa na haichukui zaidi ya dakika moja utakuwa na kadi yako tayari kwa matumizi.
Kabla hatujaendelea tufahamu kwanza Mpesa visa kadi ni nini kwa undani wake.
M-Pesa Visa kadi ni nini?
Hii ni kadi mbadala ambayo humwezesha mtu kufanya malipo mtandaoni pindi anapokuwa ananunua bidhaa au huduma yoyote mtandaoni.
Kadi hii inaruhusu kutumia pesa zako zilizopo kwenye akaunti ya M-Pesa kufanya malipo yoyote ya kidigitali bila kuhamisha pesa kwenda kwenye akaunti nyingine ya Bank bali utatakiwa kutoa pesa kutoka kwenye normal Mpesa yako kwenda kwenye kadi yako.
M-Pesa Visa Kadi siyo kadi ya mkopo bali ni kadi ya malipo inayotengenezwa kupitia njia ya Mpesa tu yaani STK, USSD na App.
Baada ya kutengeneza M-Pesa Visa Kadi utapokea ujumbe wenye taaarifa zote kuhusu kadi yako ikiwemo kadi namba, tarehe itakayo-expire, CVV (Card Verification Value) namba.
Ili uweze kufanya malipo mtandaoni ni lazima uweke pesa kwenye kadi hiyo mara tu baada ya kuitengeneza au pale unapotaka kununua kitu chochote online.
CVV ni nini?
Baada ya kutengeneza kadi utatumiwa CVV namba, je CVV ni nini? Ni namba za usalama ambazo huwasaidia wamiliki wa tovuti kuhakiki kama kweli wewe ni mmiliki halali wa hiyo kadi, pia husadia kupunguza udanganyifu unaoweza kufanyika kutoka kwenye kadi yako ya M-Pesa.
Bila CVV namba huwezi kufanya muamala wowote ule. Namba hii pia inasimama kama nywila ya kadi yako unapotaka kununua kitu mtandaoni.
CVV zinafanya kazi ndani ya dakika 30 za mwanzo baada ya malipo kufanyika, na hii husaidia kadi yako isitumiwe na mtu mwingine ambaye kwa bahati mbaya anaweza kujua taarifa za kadi yako pia asiweze kubadilisha CVV namba.
Jinsi ya Kutengeneza M-Pesa Visa Kadi Nchini Tanzania.
Fuata hizi hatua kufanikisha zoezi hili,
- Bofya *150*00#.
- Chagua namba 4 LIPA kwa M-PESA.
- Chagua namba 7 M-Pesa VISA Card.
- Chagua namba 1 Tengeneza Kadi.
- Baada ya kufanikisha kutengeneza kadi, utapokea ujumbe wenye taarifa kuhusu kadi yako.
Jinsi ya Kuangalia Huduma Mbalimbali Kwenye Kadi Yako
- Bofya *150*00#.
- Chagua namba 4 LIPA kwa M-PESA.
- Chagua namba 7 M-Pesa VISA Card.
- Baada kuchagua namba sita utaona list ifuatayo (Tengeneza kadi. Taarifa za kadi. Weka Pesa kwenye Kadi. Salio la Kadi. Kadi Yangu. Msaada.)
Kwenye M-Pesa App
- Fungua M-PESA APP.
- Chagua Services tab.
- Chagua M-PESA Visa Card.
- Bofya Tengeneza M-PESA Visa Card.
- Baada ya hapo utapokea ujumbe wenye taarifa zako za kadi.

Utofauti wa Mpesa Visa card na MasterCard
Utofauti wake ni kwamba Mpesa Visa card inatumika kufanyia malipo mtandaoni tu, mwenye uwezo wa kuweka pesa (top up) kwenye hii card ni mmiliki pekee, huwezi kutumia kadi hii kwa lengo la kutumiwa pesa kutoka upande wa pili ikiwa MasterCard inaweza kutuma na kutumiwa pesa, kufanya malipo mtandaoni na mwisho kabisa card hii ni lazima iwe inashikika.

Mpesa visa card ni kwaajili ya malipo tu.
Huduma hii ya M-Pesa na Visa nchini Tanzania inaondoa ulazima wa kuwa na akaunti ya Master card ili kufanya malipo mtandaoni kitaifa na kimataifa.
Kwa usalama zaidi, inashauriwa kurekodi maelezo ya kadi yako mahali salama na kufuta ujumbe wa nakala za Visa Kadi ya Mpesa kutoka kwenye simu yako! ili kuepusha kuvuja kwa taarifa zako za kadi hasa hasa kama simu yako inashikwa na watu wengi.
Vodacom wamerahisisha maisha kwa kuweka uhusiano huu unaowawezesha watumiaji wa M-Pesa kufanya malipo kidigitali kupitia mtandao wa Visa wenye zaidi ya wafanyabiashara milioni 100.
Hivyo ndivyo unaweza kutengeneza M-Pesa Visa Card kwa ajili ya kufanya malipo yoyote mtandaoni.
Hapo nadhan ni namba 7 badala ya namba 6.
Ni nzuri sana.
Hongera
Naona imebadilika, shukrani sana Anthon’s nimerekebisha.