Takribani wiki mbili zilizopita nilipigiwa simu na mfanya biashara mmoja akisema nimsaidie kutengeneza website. Website ambayo mtu akiitembelea awe convinced directly kuwa mteja wake, yeye yuko tayari kulipa kiasi cha pesa ilimradi tu hayo matokeo anayoyataka ayaone.
Nilijaribu kumwelekeza kuwa kwa upande wa website sisi tutafanya mikakati ya SEO kuifanya website yake ipande kwenye search engine ili mtu anapotafuta huduma unayoitoa aweze kukuona kirahisi kwenye search result ya google. Tutatoa mapendekezo maudhui yaweje kwenye website ili kuvutia zaidi.
Baada ya hapo mtu hawezi kushawishika moja kwa moja kununua huduma yako kwa kutembelea website yako tu kuna mambo mengi ambayo humfanya mteja afikie maamuzi ya kununua huduma yako ikiwemo maudhui yaliyopo kwenye website, muonekano wake lakini pia utofauti wako kwa social media (positioning).
Sababu kwenye website kuna sehemu ambayo huwa tunaweka social media links mtembeleaji aki-click hizo link je huko kwenye social media atakuona kama ulivyojionyesha kwenye website?
Je, marketing strategies zako zitamfanya mtu arudi tena kwenye website au ashawishike kununua bidhaa yako, brand yako ikoje?
Website pekee haiwezi kukufanya upate wateja mtandaoni bali itakujengea visibility shikamavu mtandaoni.
Gharama ya kutaka kuuza leo leo
Mfanya biashara anakupatia fedha kwa mashart kweli kweli: “Nataka ndani ya mwezi huu nianze kuona matokeo, nipate wateja wa kutosha, followers wengi, I want to see big numbers n.k.”
Ni kweli hakuna mtu ambaye anataka kutoa pesa yake halafu baadae asione matokeo. Hakuna. Kila mtu anataka kuona amepiga hatua kwenye kazi yake lakini ni vyema kujua ukweli kuhusu kupata wateja mtandaoni kabla hujaazimia kuanza kuuza bidhaa/huduma zako mtandaoni.
Inabidi ujue kuwa kuna mchakato hapa katikati mpaka kuwapata wanunuzi wa bidhaa yako ambao ni :
- Brand awareness (Watu wakufahamu)
- Build community (Watu wakuamini)
- Conversion (Watu wahamasike kununua)
Wengi wanakosea hapa:
Anarusha matangazo kwa media either yeye mwenyewe au marketers aliowalipa, akitarajia kupokea utitiri wa wateja. Lakini, asilimia 80 ya simu zinazopigwa zinaishia kwa watu kuuliza maswali kisha wanachikichia mitini. Kweli, idadi ya followers inaongezeka, lakini cha ajabu, mauzo hayaongezeki.
Kwenye tangazo, comments zinasoma 1k hadi 5k lakini matokeo anayoyatarajia yanagonga mwamba kila kukicha. Mteja anaanza kuwalaumu marketers kwa kushindwa kufikia matarajio yake.
Ikiwa anapata yote hayo, shida ni nini hasa?
Shida kubwa ni kwamba mfanya biashara anataka kuuza leo leo kupitia tangazo au matangazo mawili matatu aliyoyatengeneza jambo ambalo ni gumu kulifanikisha, hajui umuhimu na kujenga msingi thabiti kwenye mitandao ya kijami ili apate matokeo anayoyahitaji.
Kuanza na malengo ya haraka bila kuwekeza katika brand awareness na kujenga community ni sawa na kujenga nyumba bila msingi imara.
Watu wengi wanaweza kuona bidhaa yako lakini kama hawakufahamu au hawana imani na brand yako, hawatachukua hatua ya kununua.
Matokeo hayo yanatokana na ukosefu wa uelewa kuhusu safari ya mteja (customer journey) na jinsi inavyohusiana na mauzo.
Kwanza, ni muhimu kuhakikisha kuwa watu wanakufahamu (awareness), kisha wanakutambua na kukuamini (community building) na mwisho wanakuwa tayari kununua (conversion). Hii ni safari inayohitaji muda, uvumilivu, na mikakati sahihi.
Maudhui unayotengeneza leo yanaweza kukupa wateja wengine miezi sita ijayo. Jaribu kuliangalia soko kwa miazi sita inayokuja utakuwa katika hali gani.
Ni muhimu kujua mchakato mzima wa masoko utakaoupitia na nini kinachohitajika ili kufikia malengo yako ya kuuza mtandaoni kwa urahisi.
Mwisho
Kabla ya kurusha matangazo, ni vyema kuanza kwa kuwekeza muda na fedha katika kujenga brand awareness na community.
Hii itahakikisha wanunuzi watakapokuwa tayari wamefahamu na kukuamini basi watakuwa tayari kuchukua hatua ya kununua bidhaa au huduma yako. Mkakati huu wa hatua kwa hatua utaongeza uwezekano wa kupata matokeo ya kudumu, badala ya matokeo ya haraka yasiyo na msingi.
Mafanikio ya kweli kwenye masoko ya kidigitali hayaji bin vuu kwa usiku mmoja. Inahitaji uvumilivu na uwekezaji wa muda mrefu. Post yako leo inaweza kukuletea mteja miezi miwili ijayo lakini ukitaka kuuza leo leo utajikuta unaungana na wale wanaosema “Mitandao haisaidii”
0 Comments