Karibu tanzlite
Pata masoko kidigitali
Kuza biashara yako ifikie wateja wengi zaidi kwa kutumia majukwaa ya kidigitali kama vile mitandao ya kijamii na tovuti. Fahamu namna gani mabadiliko ya tehama yamerahisisha biashara yako kufikia wateja wengi zaidi kwa urahisi.
Huduma Kwanza, Lipa Baadaye

Kwanini sisi chaguo lako?

Huduma zetu ni bora na tumetunukiwa vyeti kutoka HubSpot na Google vya umahiri katika masoko ya kidigitali. Lengo letu ni kuhakikisha biashara yako inakua na kufikia wateja wengi kwa gharama nafuu. Soma blogu yetu kufahamu mengi. Wasiliana nasi leo tukuhudumie.

Mambo ni digitali

Kila mtu yuko online, wakiwemo wateja wako

Kama mfanyabiashara, ni lazima ufahamu njia za kisasa za kufikia wateja wako. Watu wengi wanatumia muda mwingi kwenye simu janja. Hawana muda wa kuangalia mabango tena wala kusikiliza redio. Watu wako bize online. Hivyo hakuna budi kuwafikia.
Jifunze kutoka kwetu

Endesha warsha ya Digital Marketing katika eneo lako la kazi

Je unataka kupata maarifa wewe na wafanya kazi wako juu ya mbinu mpya za kuendesha mwasailiano katika ulimwengu wa dijitiali? Tualike eneo lako la kazi upate mafunzo haya adhimu.
Huduma za Digital Marketing

Tunatoa Huduma Zifuatazo

i

Kuandaa Maudhui

Tunakuandalia maudhui kwa ajili ya kushirikisha wadau wa biashara yako. Tunaandaa makala za blogu, post za mitandao ya kijamii pamoja na maudhui ya kuweka kwenye kurasa za tovuti yako

Kuendesha Mitandao ya Kijamii

Fahamu namna ya kuongeza followers, tengeneza posts zenye kuwashirikisha followers wako.

Matumizi ya Email kwa Biashara

Fahamu namna ya kukusanya barua pepe za wadau na wateja wa biashara yako. Washirikishe kwa urahisi kupitia barua pepe.

Matangazo Mguso - Pay Per Click

Je unataka kugikia wateja sahihi kwa njia ya matangazo ya Google au Facebook? Tunaweza kukusaidia kuwalenga wateja sahihi.

Matokeo ya Haraka - SEO

Je watu hawakuoni mtandaoni? Website yako haipo miongoni mwa matekeo ya mwanzo ya search results? Tunakusaidia kuweza kuomekana kwa urahisi kwa kuamdaa mpango wa SEO.

Web Analytics - Upimaji

Kwa kutumia Analytics, tunaweza kukusaidia kutambua kipi kinafanya vizuri na kipi hakiendi vizuri katika mpango wako wa digiti.

Miliki Tovuti Yako

Ongeza umaarufu wa biashara yako kwa kufungua tovuti. Wafanye watembeleaji wa tovuti kuwa wateja wa wako.
k

Graphic Design

Tunatengeneza graphics kwa ajili ya matangazo (posters) mbalimbali. Wafurahishe wanaokutembelea (followers) mtandaoni kwa picha zilizo nakshiwa kwa umaridadi.

Amua Sasa!

Kutangaza biashara kimtandao ni njia rahisi na isiyo gharama kuwafikia watu wengi zaidi. Wasiliana nasi tukusaidie.