Wafanya biashara wengi wanatamani kuweka biashara zao Google Map ili mteja au mtu yeyote akitafuta bidhaa au huduma wanazotoa basi waonekane.
Na vitu ambavyo wengi wanatamani vionekane ni website yao (kama wana website), namba zao za simu, mitandao yao kijamii, wanapatikana wapi na wanajihusisha na nini.
Hii ni njia mojawapo ya kukuza biashara mtandaoni kupitia Google.
Katika makala hii, nitakuelekeza hatua kwa hatua jinsi ya kuweka biashara yako Google Map na jinsi ya ku-verify.
Kwanza angalia hii picha kulia. Hivyo ndivyo biashara yako inatakiwa kuonekana Google.

Hatua kwa hatua jinsi ya kuweka biashara yako Google Map
Kwanza kabisa kabla ya yote fungua Google business profile kisha bonyeza Start Now. Tuendelee
Haya ndio mambo unatakiwa kuyajua na kufuata hatua kwa hatua ili biashara yako ikubaliwe na ionekana Google.
- Jina la biashara au kampuni.
Hakikisha unaandika jina la kampuni kama lilivyosajiliwa BRELA. Baada ya kuwa verified ndio unaweza kuja kubadili lakini kwa sasa weka official name.

- Aina ya Biashara.
Utatick kibox kama unauza kupitia website, unataka wateja waje ofisini kwako au wewe ndio unawatembelea wateja wako.
Mara nyingi wengi ofisi za bongo zinataka wateja wafike ofisini kwa hiyo “Tick vyote”.

- Taarifa za kampuni/Biashara.
Jaza hizi taarifa vizuri: Nchi, Mtaa biashara ilipo, anuani ya eneo hilo (Postal Code) na Mkoa. Zijaze hizo taarifa kwa usahihi usikosee.
Ukikosea hapo kwenye Map itakuja isome kwingine kabisa na itakusumbua.

Bonyeza next. Hapo mbele utaletewa option uangalie kama biashara yako ipo au la, ikiwa haipo cha kufanya we shuka mpaka chini palipo andikwa “None of these” halafu click Next.
- Ramani.
Hiki ni kipengele muhimu sana kwa sababu ramani utakayoiweka ndio itakayoonekana Google, mtu yeyote anaweza kuifuata ikamfikisha hadi hapo ofisini kwako
Hakikisha inapoint ofisi yako ilipo exactly tofauti na hapo itakuwa inawapeleka watu sehemu nyingiine.
- Mawasiliano.
Namba ya simu itakayoonekana Google. Hiyo namba inakuwa public mtu yeyote duniani anaiona na kuwapigia akitaka.
Hadi hapo utakuwa umemaliza zoezi na utapokea ujumbe kwenye email yako kuthibitisha kwamba Google Business profile iko verified au la!
Changamoto inayowakuta wengi wakati wa kuweka biashara Google Map
Watu wengi wanashindwa kuweka biashara zao Google kwa sababu hawajui nini wafanye au kitu gani kinahitajika. Ndio maana Google huwa wana kataa ku verify maombi yao.
Hii imenitokea mimi mwenyewe, nilienda kwa mteja pale Ilala karibu na Amana Hospital kumtengenezea Googe Business Profile ili biashara yao ionekana google.
Nilijaribu kuiweka biashara yao Google lakini Google walikataa mara mbili mfululizo kwa sababu kuna vitu sikuweza ku virekodi kama inavyohitajika na ilinichukua takribani wiki mbili.
Uki tuma video leo ili ifanyiwe verification inachukua takribani siku tano – ndani ya hizo siku tano au kabla watakwambia kama iko verified au la!. Mara nyingine huchukua dakika tano tu.
Haya ndio majibu niliyopewa na Google baada ya kurekodi na ombi langu likakataliwa.

Ufanye nini kama biashara yako itagoma kuwa verified?
Kwako wewe unaweza ukafanya hivyo vyote nilivvyoviweka hapo juu na biashara isiwe verified na Google. Itakuletea ujumbe wa “Your business is not visible to customers”

Baadhi ya biashara zinahitaji u rekodi video fupi ya dakika 2 ya eneo ilipo biashara yako ili Google wajiridhishe kama kweli ni wewe ni mmiliki halali wa biashara na ni biashara kweli? au la!
Jinsi ya ku-Verify Google Business Profile kwa Video
Mwanzoni sijakwambia kuhusu kuchagua njia gani utatumia ili uwe Verified.
Njia ya kwanza ni namba ya simu kama nilivyokuonyesha hizo process hapo juu lakini kwa makampuni njia ambayo huwa inatumika ku verify mara nyingi ni VIDEO au Email.
Napendekeza u verify kwa njia ya video, Ikikubaliwa sawa ila isipokubaliwa utaona ujumbe unaosema “verification not successful. To get verified submit another video“ (angalia picha hapa juu). Bonyeza Review issues
Utaona ni kitu gani haujakirekodi vizuri so vitu vyenyewe kwa ujumla ni kama ifuatavyo.
- Street Sign, Recognizable landmark, Neighbouring business.
Mfano bango linaloonyesha jina la mtaa, clock tower au kitu chochote maarufu kinachojulikana na kipo Google tayari. Ikiwa hivyo vyote hakuna basi rekodi bango linaloonyesha biashara yoyote iliyopo karibu na pia tayari wameshaiweka Google.
- Permanent Sign.
Kwenye hiyo biashara yako kama kuna mabango au umeandika ukutani hakikisha pia unayarekodi.
- Rekodi unavyofungua ofisi.
Hii inaonyesha kuwa wewe ndiyo mmiliki halali wa hiyo biashara siyo kila mtu ana funguo za hapo ofisini.
Kwa sababu kwenye ku rekodi utaanzia nje mdogo mdogo unarekodi hadi unaifungua mlango unaingia ndani (hakikisha ofisi iwe imefungwa na kufuli au kitasa kabla hujaanza kurekodi) Ukifika mlangoni rekodi jinsi unavyofungua.
Zoezi hili lifanye ndani ya dakika 2 tu kisha Submit.
Kwa kifupi anza kurekodi mazingira ya nje (street sign/neighbouring business), kama kuna mabango mmeyaprint nje au ukutani hadi unafungua mlango, mazingira ya mule ndani ofisni.
Rekodi vizuri vitu vyote vitatu kama nilivyoviorodhesha hapo juu. Usirekodi mtu yeyote ukiwa unafanya hivyo.
Mwisho
Hongera umeweza kutengeneza njia moja wapo ya kupata wateja mtandaoni kupita Google. Kilichobaki ni wewe kuhakikisha unaweka taarifa zote unazotaka ziwepo google kwa usahihi. Kuandika posts mara kwa mara, kuongeza au kupunguza picha, kuomba reviews n.k
Kwa msaada na maelezo mengine nicheck Whatsapp







0 Comments