Jinsi ya Kutumia WhatsApp Business Kukuza na Kutangaza Biashara Yako
Mtandao wa WhatsApp umetutoa mbali sana. Kutoka kwenye status za kuandika mpaka status za picha na video. Kutoka kwenye magrupu yenye ukomo wa watu 60 mpaka sasa magrupu ya watu nyomi hadi 257.
Ni wazi kwamba mtandao wa WhatsApp umezidi kuwa bora ili kuendelea kuwafurahisha watumiaji wake. Bora ukose application zingine kwenye simu lakini si WhatsApp.
WhatsApp imekuwa zaidi ya sehemu ya kuchat na kutumiana jumbe zenye kufurahisha (meme), bali ni fursa ya kibiashara kwa wajanja.
Watu wanataka kuuza, watu wanataka kujiweka karibu na wateja wao. Wengine ndio kwanza wanafungua biashara zao wakitafuta namna ya kujitangaza. WhatsApp imekuwa kimbilio la wajasiriamali wengi wa kitanzania.
Watu wameanzisha magrupu ya WhatsApp kwa lengo la kuendesha semina na mafunzo mbalimbali. Kuendesha vikundi vya kukopeshana, maarufu kama ‘vikoba’. Vilevile magrup haya yanatumika kuhamasisha watu kujumuika kwenye matamasha na warsha mbalimbali.
Siku hizi hata vikao vya Sendoff na harusi vinaendeshwa kwenye magrupu ya WhatsApp. Kama bado umejiunga kwenye magrupu ya kipuuzi, basi umebaki wewe tu na wapuuzi wachache. Wenzako tunasaka fursa!
Yani siku hizi kupata namba ya mtu ni rahisi sana kwa sababu anajua baadaye utaona matangazo ya biashara yake kwenye status. Wala si kwa ubaya, ni katika harakati za kutafuta masoko na kujipatia riziki. Wewe ambaye huna cha kutangaza usione kero.
Hatufahamu ni mazuri yapi mengine wamiliki wa mtandao wa WhatsApp wametuandalia, lakini kizuri kimojawapo ni kuhusu application ya WhatsApp Business.
WhatsApp Business ni nini na ina tofauti gani na WhatsApp ya Kawaida?
Kwanza kabisa, WhatsApp Business ni application halali inayomilikiwa na kampuni ya WhatsApp Inc. Hii sio kama zile WhatsApp GB na zinginezo (not a third-part App) ambazo huwa zinakataliwa. Hii ni maalumu kwa wafanya biashara na wajasiliamali wanaotaka kupromote biashara zao pamoja na kuimarisha mahusiano na wateja wao. Lakini hata wewe usiye na biashara unaweza kuitumia kwa mawasiliano ya kawaida.
Makampuni kama Bloomberg na Mwananchi wanatumia WhatsApp Business API (huduma advanced hii ni huduma ya kulipia) kutuma updates kwa subscribers wao moja moja kwenye inbox zao.
Sasa tuiangalie WhatsApp Business kiundani zaidi. Vitu ambavyo utavipata ndani yake ni kama ifuatavyo;.
- Business profile
- Ujumbe automatic wa salamu
- Customer Management
- Takwimu/statistics
- Majibu ya haraka (quick replies)
Business Profile
Ukiangalia profile ya mtu anayetumia WhatsApp Business utaona ina muonekano tofauti na ile ya kawaida. Hapa utaona vitu kama jina la biashara, maelezo ya biashara (business description), location pamoja na siku na masaa anayofungua biashara yake. Hivi ni vitu ambavyo huwezi kuviona kwa mtu anayetumia WhatsApp ya kawaida.
Customer Management
Hapa unaweza kuchambua na kupangilia namba za WhatsApp ulizonazo katika makundi mbalimbali ya wateja. Kwa mfano unaweza kumwekea alama (label) kama vile mteja mpya, aliyelipa, asiyelipa, aliyetoa oda mpya na aliyemaliza oda yake.
Ujumbe Automatki wa Salamu
Hapa unaweza kutengeneza ujumbe wa salamu utakao kuwa ukitumwa kwa kila anayekutumia meseji. Ili kuondoa kero na usumbufu, ujumbe huu hutumwa endapo tu hamjawasiliana kwa kipindi cha siku 14. Ujumbe huu wa salamu unaweza kuwa unaelezea kwa ufupi juu ya shughuli unayofanya. Ni namna ambavyo wewe utapenda iwe.
Takwimu
Katika application ya WhatsApp Business, unaweza kupata takwimu kuhusu meseji ulizotuma. Utaweza kuona idadi ya meseji ulizotuma, zilizofika na zilizosomwa.
Quick replies and away message
Sikushauri utumie sana hii feature kwani humfanya mtu ajisikie kama ana wasiliana na roboti badala ya mtu. Kama namba yako ya mawasiliano ya kawaida ndiyo hiyo hiyo unatumia kwa biashara zako bora usitumie hii setting kwani si kila mtu ni mteja wako.
Jinsi ya kuwezesha WhatsApp Business
Ni rahisi sana kuseti business profile kwenye application ya WhatsApp Business. Unachotakiwa kufanya ni kwenda Playstore ama Appstore na kudownload WhatsApp Business. Baada ya hapo fungua application na uende kwenye Settings.
Kama unatumia android bofya kwenya vidoti vitatu upande wa juu kulia > Settings > Business settings > Hapo utaona setting zote unazotaka kufanya.
Mwisho…
Dunia ya sasa ni dunia ya kujiuza (simaanishi kujiuza unakofikiria wewe). It is all about branding yourself. Kama hutokuwa na ujasiri wa kusimama na kuonyesha ujuzi na maarifa yako, unataka nani akufanyie hivyo?
WhatsApp ni moja kati ya jukwaa zuri kuji-brand. Mara moja moja si mbaya kupost utani (meme) lakini isiwe kila siku wewe ni wa kupost upuuzi tu. Usifikiri ni utani tu, people are more likely to associate you with the things you post online. Jenga taswira chanya ili uweze kuvuta fursa zije upande wako.
Unatuamiaje WhatsApp yako? Tuambie uzoefu wako.