Jinsi ya Kutumia WhatsApp Business Kukuza na Kutangaza Biashara Yako

mwanamke akitumia whatsapp

Written by Shukuru Amos

I am the founder of Tanzlite Digital, Creator, Author of Mbele Ya Muda, and the most followed Tanzanian marketer on LinkedIn.

Posted December 10, 2019

Mtandao wa WhatsApp umetutoa mbali sana. Kutoka kwenye status za  kuandika mpaka status za picha na video. Kutoka kwenye magrupu yenye ukomo wa watu 60 mpaka sasa magrupu ya watu nyomi hadi 257. 

Ni wazi kwamba mtandao wa WhatsApp umezidi kuwa bora ili kuendelea kuwafurahisha watumiaji wake. Bora ukose application zingine kwenye simu lakini si WhatsApp.

WhatsApp imekuwa zaidi ya sehemu ya kuchat na kutumiana jumbe zenye kufurahisha (meme), bali ni fursa ya kibiashara kwa wajanja. 

Watu wanataka kuuza, watu wanataka kujiweka karibu na wateja wao. Wengine ndio kwanza wanafungua biashara zao wakitafuta namna ya kujitangaza. WhatsApp imekuwa kimbilio la wajasiriamali wengi wa kitanzania. 

Watu wameanzisha magrupu ya WhatsApp kwa lengo la kuendesha semina na mafunzo mbalimbali. Kuendesha vikundi vya kukopeshana, maarufu kama ‘vikoba’. Vilevile magrup haya yanatumika kuhamasisha watu kujumuika kwenye matamasha na warsha mbalimbali. 

Siku hizi hata vikao vya Sendoff na harusi vinaendeshwa kwenye magrupu ya WhatsApp. Kama bado umejiunga kwenye magrupu ya kipuuzi, basi umebaki wewe tu na wapuuzi wachache. Wenzako tunasaka fursa! 

Yani siku hizi kupata namba ya mtu ni rahisi sana kwa sababu anajua baadaye utaona matangazo ya biashara yake kwenye status. Wala si kwa ubaya, ni katika harakati za kutafuta masoko na kujipatia riziki. Wewe ambaye huna cha kutangaza usione kero.

Hatufahamu ni mazuri yapi mengine wamiliki wa mtandao wa WhatsApp wametuandalia, lakini kizuri kimojawapo ni kuhusu application ya WhatsApp Business.

WhatsApp Business ni nini na ina tofauti gani na WhatsApp ya Kawaida?

Two whatsapp icons

Kwanza kabisa, WhatsApp Business ni application halali inayomilikiwa na kampuni ya WhatsApp Inc. Hii sio kama zile WhatsApp GB na zinginezo (not a third-part App) ambazo huwa zinakataliwa. Hii ni maalumu kwa wafanya biashara na wajasiliamali wanaotaka kupromote biashara zao pamoja na kuimarisha mahusiano na wateja wao. Lakini hata wewe usiye na biashara unaweza kuitumia kwa mawasiliano ya kawaida.

ALSO READ:  Jinsi Ya Kumsaidia Mjasiriamali Mdogo Kukuza Biashara Yake Mtandaoni

Makampuni kama Bloomberg na Mwananchi wanatumia WhatsApp Business API (huduma advanced hii ni huduma ya kulipia) kutuma updates kwa subscribers wao moja moja kwenye inbox zao.

Mtandao wa WhatsApp umekuwa kimbilio kwa wajasiriamali wengi nchini Tanzania.

Sasa tuiangalie WhatsApp Business kiundani zaidi. Vitu ambavyo utavipata ndani yake ni kama  ifuatavyo;.

  • Business profile 
  • Ujumbe automatic wa salamu
  • Customer Management
  • Takwimu/statistics
  • Majibu ya haraka (quick replies)

Business Profile

Ukiangalia profile ya mtu anayetumia WhatsApp Business utaona ina muonekano tofauti na ile ya kawaida.  Hapa utaona vitu kama jina la biashara, maelezo ya biashara (business description), location pamoja na siku na masaa anayofungua biashara yake. Hivi ni vitu ambavyo huwezi kuviona kwa mtu anayetumia WhatsApp ya kawaida.

Customer Management

Hapa unaweza kuchambua na kupangilia namba za WhatsApp ulizonazo katika makundi mbalimbali ya wateja. Kwa mfano unaweza kumwekea alama (label) kama vile mteja mpya, aliyelipa, asiyelipa, aliyetoa oda mpya na aliyemaliza oda yake.

Ujumbe Automatki wa Salamu

Hapa unaweza kutengeneza ujumbe wa salamu utakao kuwa ukitumwa kwa kila anayekutumia meseji. Ili kuondoa kero na usumbufu, ujumbe huu hutumwa endapo tu hamjawasiliana kwa kipindi cha siku 14. Ujumbe huu wa salamu unaweza kuwa unaelezea kwa ufupi juu ya shughuli unayofanya. Ni namna ambavyo wewe utapenda iwe. 

ALSO READ:  Scam Alert: Tanzlite is NOT hiring online employees for part-time, and we don't have any foreign representative

Takwimu

Katika application ya WhatsApp Business, unaweza kupata takwimu kuhusu meseji ulizotuma. Utaweza kuona idadi ya meseji ulizotuma, zilizofika na zilizosomwa.

Quick replies and away message

Sikushauri utumie sana hii feature kwani humfanya mtu ajisikie kama ana wasiliana na roboti badala ya mtu. Kama namba yako ya mawasiliano ya kawaida ndiyo hiyo hiyo unatumia kwa biashara zako bora usitumie hii setting kwani si kila mtu ni mteja wako.

Jinsi ya kuwezesha WhatsApp Business

Ni rahisi sana kuseti business profile kwenye application ya WhatsApp Business. Unachotakiwa kufanya ni kwenda Playstore ama Appstore na kudownload WhatsApp Business. Baada ya hapo fungua application na uende kwenye Settings.

Kama unatumia android bofya kwenya vidoti vitatu upande wa juu kulia > Settings > Business settings >  Hapo utaona setting zote unazotaka kufanya.

Mwisho…

Dunia ya sasa ni dunia ya kujiuza (simaanishi kujiuza unakofikiria wewe). It is all about branding yourself. Kama hutokuwa na ujasiri wa kusimama na kuonyesha ujuzi na maarifa yako, unataka nani akufanyie hivyo?

WhatsApp ni moja kati ya jukwaa zuri kuji-brand. Mara moja moja si mbaya kupost utani (meme) lakini isiwe kila siku wewe ni wa kupost upuuzi tu. Usifikiri ni utani tu, people are more likely to associate you with the things you post online. Jenga taswira chanya ili uweze kuvuta fursa zije upande wako.

Unatuamiaje WhatsApp yako? Tuambie uzoefu wako.

TANGAZO: Tumeanzisha group la WhatsApp kusaidia wajasiriamali wanaouza bidhaa mtandaoni. Bofya picha hapo chini.

7 Comments

  1. Balbina

    Hii imekua useful sana. Asante mwandishi

    Reply
    • Shukuru Amos

      Thank you Balbina, endelea kufuatilia makala zetu ili kufahamu zaidi namna ya kukuza biashara yako kidigitali.

      Reply
  2. Mnkeny Endrew Emmanuel

    Like it

    Reply
  3. Joseph mathei

    Nimependa Sana mafunzo haha ntazidi kuyafutilia zaidi ili nijue jinsi yakutumia Whatsapp business.

    Reply
  4. Dickson Kisaka

    Ningependa kujua,je,kama niliitumia kutangaza biashara ya kwanza nikaachana nayo nataka nitumie biashara nyingine na watu wengine. Je itafaa kutumia namba hiyo hiyo na wale wakwanza wasinipate?

    Reply
    • Shukuru Amos

      Unaweza kutengeneza group jipya la WhatsApp na kuwajulisha uliokuwa nao kwenye group la biashara nyingine. Au kama ulikuwa na unaweka bidhaa kwenye status, unaweza kuwaandikia kwamba umebadili biashara.

      Reply

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

You May Also Like

Products From Tanzlite