Jinsi ya Kuomba Passport ya Kusafiria Tanzania 2026

Jinsi ya kuomba passport ya kusafiria Tanzania

Written by Anthony Charles

Anthony Charles is a young web designer | Content writer. He build websites for business growth.

Posted March 5, 2026

Kupata Passport ya kusafiria Tanzania ni mchakato wa takribani wiki mbili unakuwa umepata passport yako lakini inaweza kwenda hadi miezi miwili au mitatu kwasababu mbali mbali kama ilivyokuwa kwangu. 

Iwe unataka kusafiri kikazi, kimasomo, au unatafuta kitambulisho cha kimataifa ili kuhakiki akaunti zako (Verification), kufahamu hatua kwa hatua nini kinahitajika, mchakato wake ukoje mwanzo mwisho ni jambo la msingi sana. 

Katika mwongozo huu, nitakueleza kila kitu unachopaswa kufahamu kwa sababu mimi mwenyewe nimefanya, kwa ufupi gharama ya serikali ya kuomba passsport ni Tsh 150,000/=  ila wewe hakikisha una bajeti ya 200,000/=

Kwa nini niliamua kutafuta Passport?

Watu wengi huanza kutafuta passport wakiwa na safari tayari, lakini kwangu ilikuwa tofauti. Kitu kilichonisukuma zaidi ni hitaji la ku-verify akaunti yangu ya LinkedIn. Licha ya kuwa na kitambulisho cha NIDA, LinkedIn wanahitaji Passport pekee. 

Hapo ndipo nilipoingia kwenye mchakato huu na kujifunza mengi ambayo nitakushirikisha hapa ili wewe usipate tabu niliyopata mimi.

Vitu 6 unavyotakiwa kuwa navyo kabla ya kuomba Passport 

Haya ndiyo yaliyoniwezesha mimi kupata passport. 

  1. Cheti cha kuzaliwa cha kwako. 
  2. Namba ya NIDA
  3. Cheti cha Kuzaliwa cha Mzazi mmoja wapo (Au Kiapo cha Uraia – Affidavit). 

Mara nyingi wazazi wetu hawana vyeti vya kuzaliwa, cha kufanya hapo nenda kwa Mwanasheria yeyote atakuandikia hicho kiapo kinachoonyesha Mzazi wako ni Mtanzania. Hakikisha taarifa unazotoa ni za kweli.  

Wanasheria wanajua watakuandikia vizuri. Kuhusu pesa mfano mimi Mwanasheria wangu aliniambia 20,000/= ambayo ni kawaida ikizidi hapo umepigwa (Makubaliano). 

Ni vizuri pia uwe na copy ya kadi ya NIDA ya mmoja wa wazazi wako. Itoe copy utaiambatanisha baadae. Ni njema zaidi ikiwa ya mama.

  1. Barua ya Utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa.

Nenda serikali ya mtaa waambie wakupe form ya utambulisho, utaijaza au watakusaidia kuijaza na watakupatia. 

Kuhusu pesa haizidi 4,000/= ikizidi umepigwa, wengine huwa ni bure inategemea unaisha sehemu ipi. 

  1. Passport size moja.

Kama hauna basi mwambie jirani yako au rafiki yako akupige ama uenda kwa wanaopiga Pasipoti utachagua mwenyewe kipi bora ila mimi nilipiga kwa simu yangu nika-crop biashara ikaishia hapo. 

Hii passport utaitumia tu kwenye kufanya maombi online lakini itakayoonekana baada ya passport kutoka ni ile utakayopigwa siku ukienda uhamiaji. 

  1. Barua ya Maombi Binafsi (Inayoelezea sababu ya kusafiri)

Hii ni tofauti na barua kutoka serikali ya mtaa. Hii inatakiwa iwe fupi hata aya moja inatosha kama zile tulizokuwa tunaandika kipindi kile tuko form two. 

Angalia mfano hapa

Hii ni lazima uiandike mwenyewe kwa kutumia laptop au uende stationary wakupige hela au unasemaje!. 

NB: Hapa usidanganye kama kweli unasafiri maana unaweza kukamatwa huko, kwenye maombi umeandika unaenda kusoma/kutembea halafu ukakutwa unafanya biashara aisee mimi simo kwenye hiyo kesi yako. 

Hivi ndio vitu pekee vilivyoniwezesha mimi kupata passport. Bila hivi utakuwa bado hujatimiza vigezo vya kufanya maombi ya Passport Uhamiaji. 

Hatua kwa hatua jinsi ya kuomba passport kwenye mfumo wa Uhamiaji Tanzania

Hii ni hatua ya kwanza ambayo unatakiwa uifanye ukiwa popote. Usiende ofisi za uhamiaji mfano pale ofisi za uhamiaji kurasini, Dar es Salaam kabla haujamaliza maombi ya awali kwenye mfumo.

Kama huniamini jifanye kama hujasoma hii uende utanikumbuka baadae. 

Ni vizuri utumie laptop au Desktop ukiwa unafanya maombi online maana kwenye simu itakusumbua bure. 

Bonyeza hii link Apply passport itakupeleka kwenye website ya uhamiaji tayari kwa kuanza maombi. Kama hujajisajiri jisajiri na kama tayari basi utaweka namba ya simu na kumbumbuku namba yako. 

Hapa naomba tuelewane kumbukumba namba utakayopewa hakikisha unainakiri sehemu maana utaulizwa karibia kila sehemu utakayoenda hata kwenye mfumo wa uhamiaji uki log out itakuomba hiyo kumbumbuku namba. Ukiisahau umeisha narudia ukiisahau umeisha. 

Vipengele Muhimu kuvifahamu ukiwa unajaza taarifa zako 

Jaza kila sehemu taarifa sahihi kwenye hiyo form. Vitu vichache ambavyo utakutana navyo na huenda usivielewe ni hivi vifuatavyo.  

  1. Namba ya Uraia – hii ni namba ya NIDA

  1. Kazi

Hapa andika cheo chako. Hakikisha una ushahidi usibuni cheo maana kule uhamiaji ukienda wanaweza kukuomba ushahidi. 

Mfano mimi niliandika Freelancer kwako wewe weka cheo chako. Hakikisha tu unachoandika ndio kazi yako na unaweza kujitetea. 

Jaza na upload vitu vinavyohitaji sehemu husika kama nilivyokuelekeza hapo juu hadi utakapofika sehemu ya malipo. Watakupa CONTROL number ulipie, lipia 20,000/= tu. 

Ukilipia itafunguka hiyo hatua ya mwisho. Utadownload hiyo document nzima na utaenda kui print.  

Tumemaliza hatua ya kwanza.

Hatua inayofuata ni kwenda ofisi za uhamiaji ukiwa na document zote zikiwa printed. Nisisahau, NIDA yako pia itoe copy na uiambatanishe. 

Ukifika ofisini ulizia sehemu unaweza pata Muhuli wa mwanasheria hapo hapo uhamiaji utaonyeshwa na watakupangia document zako vizuri. Gharama ya muhuli ni 10,000 sidhani kama itazidi hapo ikizidi umepigwa. 

Baadae utaziwasilisha hizo document zote zitakaguliwa kisha utapewa control number ulipie 130,000/= kwa passport ya kawaida.

Mpaka hapo utakuwa tayari umemaliza zoezi utakusanya hizo documents baadae utaitwa utaulizwa maswali ya hapa na pale, utaenda kupigwa picha na utaambiwa siku ya kwenda kuichukua na ni sehemu gani. Ni hivyo tu simple! 

Hakikisha unawahi kwenye ofisi zao maana watu ni wengi saa moja kamili asubuhi uwe umefika.

Itachukua muda gani kupata kupata Passport yangu

Kitaalamu huwa inachuua siku 14 tu  lakini kwangu ilikuwa tofauti imenichukua miezi mitatu kuipata. Tarehe ambayo niliambiwa nikaichukue pale Wizara ya Mambo ya ndani nilikuta bado haijatoka nikapigwa kalenda.

Kwako wewe ukiambiwa ukachukue tarehe fulani halafu hiyo siku ukaenda na ukaambiwa haijatoka hapo ongeza mwezi mmoja ndio uende tena vinginevyo utakuwa kama umeajiriwa pale. 

Aidha ikiwa una uharaka wa kusafiri na ushahidi unao mfano tiketi ya ndege, barua ya ajira au masomo basi unaweza kuipeleka ofisi ya uhamiaji kuomba upatiwe Passport kwa uharaka. Hii itakuokoa kuliko kusubiri.

Kama utakuwa na nyongeza ama swali lolote uliza hapa hapa au nichek WhatsApp HAPA tupange ni nchi gani tuende mwaka huu.  

Share this on

0 Comments

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Also Read

0 Comments

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.