Ifahamu kazi ya Social Media Manager na majukumu yake

hands using smartphone with laptop on the table

Written by Shukuru Amos

I am the founder of Tanzlite Digital, Creator, Author of Mbele Ya Muda, and the most followed Tanzanian marketer on LinkedIn.

Posted September 17, 2019

Mwanafalsafa maarufu wa Kijerumani, Karl Marx aliwahi kuonya kwamba teknolojia itakuja kuondoa kazi wanazofanya watu. Kwamba watu watakuwa hawana kazi za kufanya.

Hivi karibuni kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, imedhihirika kuwa maono ya msomi huyu hayakuwa sahihi.


Ni kweli kwamba teknolojia imechukua kazi nyingi zilizokuwa zikifanywa na binadamu hasa zile zenye uhitaji mdogo wa kufikiri kama vile kubeba mizigo viwandani. Siku hizi kuna maroboti yanayofanya kazi kwa ufanisi na kwa muda bila kuchoka kuliko binadamu.

Lakini pia kuna ukweli mwingine. Teknolojia imetengeza na kuboresha kazi nyingi zaidi kulinganisha na zile ilizoziondoa. Mojawapo ni hii kazi inaitwa Social Media Marketing. Mtu anayefanya kazi hii anaitwa Social Media Manager, au Social Media Coordinator.

Ulishawahi kujiuliza ni nani huwa anapost kwenye account ya Instagram ya BBC, Millardayo au account za taasisi kama UNICEF? Basi hiyo ndiyo kazi yenyewe tunayoizungumzia hapa.

Social Media ni kipengele mojawapo muhimu katika suala zima la digital marketing.

Kutokana na kukua kwa matumizi ya mitandao ya kijamii miongoni mwa watu, imeweza kushawishi watu na biashara zao kuingia kwenye Social Media kwa lengo la kushirikiana na kukuza uhusiano na wateja wao pamoja na kupata wateja wapya.

ALSO READ:  Je, ChatGPT Inaweza Kudukua Taarifa Zako?

Majukumu ya Social Media Manager

Majukumu ya social media manager ni pamoja na kusimamia na kuendesha akaunti za mitandao ya kijamii ya kampuni au watu maarufu celebrities. Haya ni baadhi ya majukumu muhimu;

  • Kuandaa maudhui (picha, video, maneno) kwa ajili ya kusambaza kwenye mitandao ya kijamii
  • Kujibu comments na maswali ya followers
  • Kushiriki (engage) na wafuatiliaji (followers) kwa niaba ya kampuni
  • Kuandaa promosheni na matangazo ya kulipia (campaigns) ili kufika watu wengi mtandaoni.
  • Kukuza jina la brand au kampuni
  • Kujenga na kuimarisha mahusiano mazuri baina ya kampuni na wateja wake
  • Kuvutia wateja kufuatilia tovuti za kampuni (lead generation)

Ifahamike kwamba kwenye kazi za Social Media, majukumu ya Social Media Manager, Social Media Specialist na Social Media Strategist yanatofautiana. Lakini kwenye makampuni madogo madogo hasa hap Tanzania unaweza ukajikuta unavaa kofia zote hizi peke yako.

Vigezo na mambo muhimu ya kuzingatia ukiwa Social Media Manager

Hauhitaji kuwa na degree kufanya kazi hii, japo baadhi ya waajiri wanaweza kupendelea mtu mwenye elimu ya juu. Jambo zuri ni kwamba unaweza kujifunza mtandaoni kuhusu maarifa haya na kuwa vizuri katika kazi yako.

ALSO READ:  The Killer Digital Strategy: Founder plus Brand Marketing

Lakini mambo muhimu katika kazi hii ni kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu mitandao mbalimbali ya kijamii. Mitandao hii inatofautiana kuanzia aina ya maudhui na watumiaji wake. Kwa Mfano Instagram ni mtandao unaopendwa na vijana, lakini mtandao kama LinkedIn ni jukwaa la wasomi. Kufahamu tofauti hizi kunakuwezesha kujua mbinu za kuwakilisha maudhui kulingana na jukwaa husika.

Mitandao ya kijamii ni watu. Kama unavotakiwa ujifunze kuishinna watu katika maisha halisi basi ndivyo ilivyo pia ukiwa online. Isiwe kila siku unapost biashara yako tu. Watu hawapendi (don’t be too selly). Kuwa mbunifu.

Jifunze kila siku mambo mapya yanayopendwa huko mitandaoni. Usilenge kupata followers tu, bali followers ambao wako interested na unachokifanya. Ukizingatia haya utaleta matokeo yenye kuridhisha kwa mwajiri wako.

0 Comments

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

You May Also Like

Products From Tanzlite