Jinsi Nilivyopata Mteja Linkedin Nikiwa Bado Mwanafunzi

Written by Anthony Charles

Anthony Charles is a young Web Designer and Developer | Content Writer. Helping Individuals escape unemployment, SMEs grow their visibility online.

Posted June 9, 2023

Sikuwahi kuamini kama Linkedin ingeweza kunisaidia kupata mteja kwani wanafunzi wengi tunaamini mtandao pekee hauwezi kukufanya upate kazi zenye maana mpaka uajiliwe kwenye makampuni au taasisi.

Jambo ambalo linatufanya tuwe na mawazo mgando na hatimae tukose fursa zilizo ndani ya uwezo wetu.

Ilikuwaje mpaka nikapata mteja?

Kitu kilichonisadia hadi nikapata mteja ni kupitia posting zangu ambazo nilikuwa nikipost kila mara huko linkedin kulingana na tasnia yangu. 

Hali yangu ya kupost mara kwa mara ndiyo iliyojenga uaminifu, kutosahaulika na kuonekana kuwa mtu ambaye ninaweza kufanya kitu fulani. 

Hivyo, siku moja nimejichokea zangu ghafula napigiwa simu, “Hello! wewe ndiye Anthony? Yes (nilijibu), nimekuona linkedin unazungumzia mambo ya ………. Na nimeangalia kwenye profile yako umejitambulisha kama web developer, hivyo unaweza kunitengenezea website? ….”

Kuanzia hiyo siku nikaamini mambo yanawezekana endapo tu utaweka juhudi, uvumilivu na nguvu katika kile unachokipambania. Linkedin ni mtandao unaoweza kumfanya mwanafunzi apate fursa za kazi as a freelancer hata kama bado anasoma.

Ninawezaje kushiriki katika jumuiya ya Linkedin hali ya kwamba mimi ni Mwanafunzi?

Kama ninaweza kuwa online masaa mawili Instagram au facebook nikiscroll up and down, nashindwaje kuutumia muda huo kuandaa maudhui au kushiriki na wenzangu katika jukwaa la Linkedin? Ule mda ambao wewe uko Tiktok, Facebook, mimi ndo naandaa maudhui halafu baadae naingia kwenye kipindi kama kawaida.

ALSO READ:  Mbinu Mpya Ya Kupata Kazi Ukihitimu Chuo

Naweza kusema kwamba kama wewe ni mwanafunzi basi unaweza kujisogeza taratibu kwenye jukwaa hili la Linkedin, mtandao ambao unakufungulia dunia kuwa unachotaka. 

Bila shaka unatamani kujua website niliyomtengeneza mteja, haikiuchukua muda website ikakamilika nayo ni  Better Careers. Tofauti na hilo kuna watu wengi pia walionitafuta inbox hivyo kutokana na uzoefu wangu mchanga baadhi ya fursa nilichengana nazo.

Tofauti na hayo jukwaa hili limenisaidia kujifunza mambo kadha wa kadha kwa kusoma post za watu wengine, kuangalia mabadiliko ya teknolojia yanavyokwenda mbio (AI), kupitia Linkedin learning huwezi amini linkedin ndiyo mtandao ambao mimi nilianzia kusoma Web Development kipindi hicho hata opening tag <> or </> sizijui. 

Linkedin ni mtandao wa watu wenye vyeo vyao, watu wanaojua kingereza vizuri

Kipindi najiunga linkedin sikuwa naelewa wapi nianzie na wapi niishie kwa sababu ukiangalia kila mmoja kwenye post zake alikuwa anatema ng’eng’e hatari. Nikawa najisemea kimoyo moyo aisee huu utakuwa ni mtandao wa watu fulani fulani hivi wenye vyeo vyao.

 Kwa kuwa mwanzo huwa ni mgumu nikiwa kule nilikuwa kama mtazamaji, mzee wa kuscroll down and up yaani nikitaka kuandika post, hizo ng’eng’e kuzipangilia ilikuwa ni issue. 

ALSO READ:  Siri Ya Mafanikio Mtandaoni, Nunua Kitabu Hiki

Mdogo mdogo we mwendo, ayeeya mwendo nikaanza kuandika na kusoma vitabu, unaambiwa mazoea hujenga tabia, ee bwana tabia yangu ya kuandika ilianza kukua taratibu na ndipo upweke wa kusema linkedin ni mtandao wa watu wenye vyeo vyao ukanitoka. 

Unajua kule LinkedIn watu wengi wanatumia kingereza kwa sababu watumiaji wengi wa Linkedin hawajui Kiswahili lakini sasa hivi unaweza kutambaa na Kiswahili kuiteka hadhira unayoilenga.

Njia pekee itakayokusaidia wewe usiteseka na barua za internship wala usisumbuke na ajira baada ya kumaliza chuo ni Linkedin inaweza kuwa miongoni mwake.

Naitwa Anthony Charles natengenza tovuti mbalimbali | Mwandishi, pia nasaidia wanafunzi wenzangu walioko chuo kuhusu namna mbalimbali za kukabiliana na unemployment.

0 Comments

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

You May Also Like

Products From Tanzlite