Faida 5 za Kutumia Mtandao Wa LinkedIn Mbali na Kutafuta Kazi

Written by Anthony Charles

Anthony Charles is a young Web Designer and Developer | Content Writer. He Creates Clean, Responsive, and Converting Websites for Business Growth.

Posted December 7, 2023

Linkedin ni jukwaa lenye jumla ya watu wapatao milioni 950 kutoka nchi zaidi ya 200 ulimwenguni. Mtandao huu unakua kwa kasi sana kutokana na fursa mbalimbali ambazo watu wanapata hasa wanaotafuta kazi na watangaza biashara.

Kuna faida gani za kutumia mtandao wa LinkedIn?  Katika makala hii nimeelezea faida tano za kutumia mtandao wa LinkedIn mbali na kutafuta kazi kama ilivyozoeleka kwa wengi.

Kujifunza.

Watu wengi wanajiunga LinkedIn kwa lengo la kutafuta kazi tu hasa vijana wanaomaliza vyuo, jambo ambalo linafanya baadhi yao kuja na mabango ya “Hi everyone, I am looking for new role and would appreciate your support. Thank you in Advance for any connection” baada ya hapo haonekani tena.

LinkedIn ni jukwaa linalokuwezesha wewe kujifunza mambo mengi yamkini hata yale uliyokuwa huyajui kutoka kwa wataalamu tofauti tofauti mfano HR, Engineer, Writers, Consultants, Career coach, Doctors, Marketers n.k wote hawa wako Linkedin. 

Uzuri ni kwamba watu hawa hufundisha mambo kadha wa kadha ikiwemo mambo gani ufanye na yapi usifanye kulingana na tasnia zao. 

Mfano HR wanafundisha jinsi ya kujibu maswali ya interview ambayo mara nyingi watahiniwa huulizwa wakiwa kwenye chumba cha mahojiano (Interview)  kama vile “Unafikiri ni kwa nini wewe unafit kwenye hii kazi, tueleze wewe ni nani, tuulize swali kama una swali n.k”

Career Coach wanafundisha vitu ambavyo unatakiwa kujua kabla ya kwenda kwenye interview mfano “Jinsi ya kuelezea ujuzi wako, namna gani unaweza kuhama kutoka kitengo kimoja kwenda kitengo kingine bila kwenda kuongeza Masters wala kwenda kukisomea hicho kitu chuoni”.

Ukiachilia mbali hayo, Linkedin learning inakupa free courses kwa mwezi mzima wa mwanzo baada kujiunga (kusubscribe) Linkedin Premium. Ofa hii ni kwa mwezi mmoja tu baada ya hapo utatakiwa kusitisha au kulipia ili uendelee na huduma (premium). 

ALSO READ:  Digital Marketing ni nini? Haya hapa mambo muhimu ya kufahamu

Haya yote utajifunza huko huko LinkedIn, ni wewe na utayari wako wa kujifunza. 

Kuongeza marafiki wapya.

Marafiki hawa wanaweza kuwa ni wataalamu wanaokuzidi kimaarifa na kiujuzi, mnaendana au unawazidi kwa lengo la kubadilishana mawazo chanya katika tasnia zenu na pengine kufanya kazi pamoja. 

Mara nyingi urafiki huu waweza kukusaidia kutatua changamoto mbalimbali usizoweza iwe kwa kuongea nao kwenye simu, message au kukutana sehemu ili kujadili zaidi baada ya kujuana huko LinkedIn.

Amini kwamba, milima haikutani lakini ninyi mnaweza kukutana katika namna ambao hukuitengemea, “aah! Kumbe ndo wewe sikutegemea kama tutakutana”. Leo mtakutana linkedIn kesho mtakutana Arusha live, uso kwa uso na huyo ndio anaweza kuwa mwenyeji wako. 

Leo mnaweza kuchati na kushiriki kwenye mijadala yenu pale LinkedIn lakini kesho inawezekana mkafanya kazi kwenye ofisi moja.

Kukuza Jina.

Kama hujulikani kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa, kitaifa basi Linkedin inakupa fursa ya kujulikana siyo tu ngazi ya kitaifa bali ngazi za kimataifa. Linkedin inakufungulia dunia kuwa unachotaka.

Huhitaji kukwea pipa mpaka marekani ili ujulikane unahitaji kuandaa maudhui yako yenye mvuto, yenye kutatua tatizo fulani, yenye kufundisha au yenye kuburudisha. Kwa kufanya hivi watu watapata kukujua wewe ni nani na unafanya nini.

Hivyo itakuwa rahisi kwako kupewa fursa za kazi kutokana na kile unachokiandika LinkedIn kwa sababu watu tayari watakuwa wanakujua. Hiyo ndiyo maana ya kukuza jina LinkedIn.

Watu hununua kwa watu wanaowajua. Vile watu hawaamini sana mitandao itakuchukua miezi, mwaka mpaka watu waanze kukuamini na kukupa fursa au ufanye nao kazi. Kuza jina lako mtandaoni kwanza watu wakufaamu fursa za kazi zitakuja baadae. 

ALSO READ:  Fahamu Namna Nzuri Ya Kutumia Mitandao Ya Kijamii

Kukuza uandishi wako.

Baada ya kumaliza mtihani wa mwisho chuoni suala la kuandika huishia papo hapo. Pengine uandishi kwako ni changamoto sana je, ni sehemu gani unaweza kufanya mazoezi ya kujiendeleza kuandika au kufanya uandishi wako uwe umenyooka, fasaha?

Ukiniuliza mimi nitakwambia ni linkedin, kwa nini? Kwa sababu inakupa nafasi kubwa ya kuandika maneno mengi kadri uwezavyo, kuna sehemu ya posts na newsletter ambapo unaweza kuandika na kukuza uandishi wako siyo kama ilivyo X (Twitter).

Wengi hushindwa kujitosa na kiingereza chao cha you know kisa wataonekana si wasomi sana au utasikia ni vigumu sana kukaa na kuandaa maudhui kwa kuandika, practice makes more perfect anza hivyo hivyo mwisho wa siku mambo yatakaa mkao. Mchicha nao ulianza kama ua mdogo mdogo unajifunza itafika wakati wewe mwenyewe utaoni kama mchezo tu.

Ikumbukwe: Mipaka ya lugha yako mipaka ya ulimwengu wako. Kingereza ni lugha ya kimataifa, kibiashara hivyo kwa namna yoyote ile inabidi uijue. 

Kutunza kumbukumbu. 

Nadhani ulishawahi kuweka kumbukumbu zako kwenye diary, notebook au kwenye application mbali mbali pia hata Linkedin yaweza kutumika kwa miradi hiyo. Ukiweka post yako kule itakaa milele mpaka utakapoamua kuifuta mwenyewe.

Muda wowote waweza kuirejea, kujikumbushia au kutunza mawazo yako kule iwe kwenye post yako au kwa kuacha comment kwenye post za watu wengine.

LinkedIn is a note taking app.  

Mwisho, LinkedIn ni mtandao wenye faida kedekede hasa kwa mtu mmoja na kampuni kwa ujumla.

Usijifungie ghetoni au kukaa offline kisa hujapata kazi, ukiwa LinkedIn utajifunza mengi sana.

4 Comments

 1. Wiston Salvatory

  Hatari sana hii content nimeipenda sana,content fupi inayoeleweka.Inaamusha akiri kutoka uvunguni na inachangamusha kwa kweli.

  Mtu yoyote anapenda kujifunza na kupata changamoto mpya kupitia LinkedIn inaweza kumusaidia sana.

  Ongera sana Mdogo wangu Anthony Charles

  Reply
  • Anthony Charles

   Ahsante sana Wiston.

   Reply
 2. Peter Sarwatt

  Ni darasa zuri sana, wengi wapo humu bila kuyajua hayo. Pia kuna fursa ambazo zinapatikana kwa wale wenye kulipia kila mwezi, ambazo wasio lipia hawawezi kuzifikia.

  Ni vyema kwa wote kutumia nafasi zetu kuwaimba LinkedIn kuwaangalia vijana wanaiotafuta kazi wawe na punguzo maalum ili wapate uwanja mkubwa zaidi wa kujiendeleza.

  Reply
  • Anthony Charles

   Huwa wanatoa hizo punguzo mara kwa mara hasa ukishamaliza huo mwezi mmoja wa free kwa premium features. Utakuta wamekuwekea punguzo la 70% 50% 45% hadi 40%.

   Reply

Submit a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

You May Also Like

Products From Tanzlite